August 30, 2019


Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amewaambia mashabiki wa kikosi hicho wasiwe na presha watakapokutana na Zesco United kutokana na kumfahamu vizuri kocha wao, George Lwandamina ambaye amewahi kufanya naye kazi.

Mwandila ameweka wazi kuwa atatumia vitu anavyovijua kumpa bosi wake wa sasa, Mwinyi Zahera ikiwa ni sehemu ya kuwatoa wapinzani wao.

Yanga imepangwa kucheza na Zesco United ambayo kwa sasa inafundishwa na Lwandamina katika mchezo wa Hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao umepangwa kupigwa kati ya Septemba 13-15, mwaka huu.

Mwandila kwa nyakati tofauti amefanya kazi na Lwandamina, kwanza wakiwa Zesco United kisha baadaye Yanga ambapo walitwaa ubingwa wa mwisho wa klabu hiyo misimu mitatu nyuma.

Mwandila amesema kuwa kwake hana hofu ya kukutana na bosi wake huyo wa zamani kwenye mechi hiyo ambapo kwake atakuwa na kibarua cha kupambana naye kwa ajili ya kuifanikisha timu yake inapata ushindi na kusonga mbele.

“Ndiyo nimefanya kazi na Lwandamina na ninamjua vizuri kuwa mtu wa namna gani lakini kwa safari hii mimi nipo huku na yeye yupo huko. Kitu ambacho nitakifanya ni kuhakikisha timu yetu inasonga mbele kwa kufanya vizuri.

“Nitatumia kila ambalo ninalijua kuhusu mifumo na mbinu zake kwa ajili ya faida ya timu yetu, japo najua haitakuwa rahisi kwa sababu ya kutokuwa pamoja kwa miaka kadhaa lakini naamini kabisa vile ambavyo ninavijua bado anavitumia na hivyo vyote tutakaa na benchi letu la ufundi kwa ajili ya kuvijadili,” alisema Mwandila.

3 COMMENTS:

  1. Mwandila acha kutudanganya hauna mbinu yeyote unatuumiza sana ila naamn siku moja utatuachia tu Yanga yetu maana ww majukumu yako hautekelezi hasa kwenye usajili forward ambazo hazna lolote bora Tambwe aje tena haki ya Mungu

    ReplyDelete
  2. Si hoja hata kidogo. Kwani Yanga ilikuwa haijuwi uwezo na Ubutu na tekeniki za Ruvu Shooting na sote tumeshuhudia kufungwa na timu hiyo na jinsi walivo elemewa hasa mwisho WA kipindi cha pili. Inavotakiwa Ni jinsi itavojitayarisha kuikabili Zesco kuliko kujuwa Siri zao

    ReplyDelete
  3. Ufundishaji wa Zahera lazima ubadilike ama kuimprove haswa kufanya timu icheze soka la Ushirikiano na pia pasi zenye malengo na ukabaji wa pamoja. Halafu kusiwe na papara ya kuharakisha kufika mbele ili kufunga bila ya kuwa na mipango mtaendaje kama timu mkiwa mnashambulia na mkiwa mnarudi...viungo wa ushambuliaji, mawingi na wafungaji wa mbele wawe na mawasiliano watoe uchoyo wawe na utulivu kuanzia mita 20 na kuendelea wanapofika lango la adui wawe na akili namna ya kuipenya ngome ya timu upinzani....haya ndiyo makosa ya kiufundi

    MFIKISHIENI MWINYI ZAHERA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic