SIMBA wameamua kurejesha kwa jamii, ambapo kuelekea kwenye SpotiPesa Simba Wiki mashabiki wameanza kujitolea kwa jamii.
Mashabiki wameanza kujitoa kwa kutoa damu sehemu mbalimbali na zoezi hilo lilianza jana stendi ya Mbagala na Ubungo na leo linaendelea pia makao makuu ya klabu pamoja na Mbagala.
Leo Jumamosi Makao Makuu ya klabu Kariakoo na stendi ya Mbagala kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni utakuwa ni mwendelezo wa kuchangia damu.
Pia mashabiki wanawake wa Mwanza jana walitembelea hospitali mbalimbali jijini humo ili kutoa misaada.
Inajenga utamaduni wa kujitolea na hasa kwa vijana ila walitakiwa waje na kitu kipya, wenzao wameshawatangulia japo kuiga lililo zuri sio vibaya.
ReplyDeleteWao ndio ambao wameiga, hawa walishaanza kitambo kuadhimisha Simba week na matendo kama haya yamekuwa yakifanyika kila mwaka, ila wao walioanza mwaka huu hii habari yao ya mwananchi ndio waigaji. --------- KAULI MBIU-------- "IGA UFE .................
ReplyDeleteKwa nini Simba wanatoka kwenye utamaduni na jadi yao ambayo imekuwa ikienziwa miaka na miaka. Kitendo cha kuanza kuvaa Jezi za blue na Jezi za njano kimenishangaza sana. Utamaduni wa Simba ni Jezi nyekundu na nyeupe toka kipindi wanaitwa Sunderland. Au ndio tunakwenda na wakati!
ReplyDeleteHizo ni away jersey na ni matakwa ya CAF wawe na jezi neutral licha ya kuwa na jezi nyekundu na nyeupe.
ReplyDelete