UNYONGE
umeanza kutanda kwenye mioyo ya watanzania hasa baada ya kuona kwamba timu yao
pendwa namba moja imeshindwa kupata matokeo ambayo walitarajia awali kuona
inashinda kwenye ardhi ya nyumbani.
Kila mmoja
ameona na kushuhudia namna timu yetu ya Taifa ilivyopambana mbele ya Kenya
mchezo wa kufuzu michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika mwaka 2020 nchini
Cameroon pale uwanja wa Taifa.
Tumekosa
matokeo inabidi tukubali kwani mpaka dakika tisini zinakamilika ubao ulikuwa
unasomeka Tanzania ambao ni wenyeji 0 sawa na Kenya ni matokeo ya kipekee hasa
ukiwa nyumbani kwenye michuano mikubwa.
Tusisahau
kwamba kwenye mpira siku zote kuna matokeo matatu ambayo ni lazima yatokee kwa
namna yoyote ile wakati timu inacheza kwenye aina yoyote ya michuano hasa
kwenye ulimwengu wa soka.
Ushindi,
hapa kila timu na kila mwalimu anayepeleka timu yake uwanjani anaamini kwamba
kipaumbele cha kwanza ni kupata matokeo chanya yatakayowapa furaha mashabiki wa
timu pamoja na timu kiujumla.
Kufungwa
hapa ni pale ambapo timu zote huwa hazifikirii kupoteza ila kutokana na makosa
ambayo yatafanywa ndani ya uwanja yatasababisha mmoja afungwe na apoteze mchezo
wake akiwa uwanjani nayo pia ni sehemu ya matokeo.
Sare hapa
ndipo timu zote mbili zimeishia kwamba
hakuna mbabe aliyeibuka kidedea wote wametosahana nguvu na hakuna ambaye ameona
lango la mwenzake hiyo ni matokeo ambayo yanatupa picha ya kazi mpya tuliyonayo
kwenye mchezo wetu wa marudio.
Haitakuwa
kazi rahisi kupenya kwao kama ambavyo tunafikiria hivyo wachezaji mna kazi
kubwa ya kufanya kuelekea kwenye mchezo wa marudio utakaopigwa Kenya Agosti 4.
Kushindana
lazima kuendelee kwa wachezaji kuhakikisha kwamba wanafikia malengo ambayo
waliyaweka awali na hakuna haja ya kukata tamaa kwani muda bado unaruhusu
kupata matokeo chanya ugenini.
Kila kitu
kinawezekana kwenye uwanja wa mpira hasa ukizingatia kwamba mpira ni sayansi na
mbinu hakuna jambo jingine ambalo linabeba mafanikio kwenye mpira zaidi ya
mipango makini kufikia mafanikio.
Kama
ilivyokuwa kwa wenyeji wa michuano ya Afcon Misri walipoteza mbele ya Afrika
Kusini nao wakawa watazamaji kama watu wengine kwenye michuano ya Afcon ambayo
ilifanyika nyumbani kwao hivyo nasi tunaweza.
Kuelekea
kwenye mchezo wa marudio wachezaji wanapaswa wabadili mbinu wasiende kujilinda
pekee bali wafunguke kutafuta matokeo chanya hasa bila kusahau kuwa na mikakati
ya kulinda na lango lao pia.
Tujipange
mwanzo mwisho huku tukiamini kwamba hakuna jambo baya kama kukata tamaa mapema
kabla hata mchezo haujachezwa tuamini kwamba uwezo wetu ni mkubwa na wachezaji
wetu tayari wameshaanza kuzoena pamoja
na kujua kile ambacho wanatakiwa kukifanya.
Ninaamini sare
waliyopata nyumbani si matokeo mabaya
ambayo yanapaswa kubezwa wamejitahidi kwa kiasi chake wachezaji wetu licha ya
kwamba hesabu zetu ilikuwa ni kupata ushindi.
Kinachotakiwa
kwa sasa ni kurekebisha makosa ambayo tumeyafanya mwanzo kwenye mchezo wetu wa
nyumbani na kwenda tukiwa na mipango mipya ya kupata matokeo ugenini nafasi
yetu ya kushinda ndio hii.
Kujiamini
kwa wachezaji kutasaidia kubadili mbinu pia na kuwafanya wacheze kwa kujituma
mwanzo mwisho hivyo wanapswa wajengwe kisasikolojia kujega muunganiko mzuri na
makini huku malengo makubwa ikiwa ni kufuzu kushiriki Chan.
Yatupasa
kujua kwamba nini tumekifuata nchini Kenya na kujituma kwa kupambana hasa
katika mchezo wetu wa marudo ambao ni muhimu kwetu kushinda ili kusonga mbele
kawenye michuano hii ambayo inawahusu wachezaji wa ndani.
Benchi la
ufundi nina amini limeona mapungufu ya timu yetu na kuyafanyia kazi ili kupata
matokeo mazuri kwenye mchezo wa marudio tunaamini kwamba bado mashabiki wapo
bega kwa bega na timu ya Taifa hivyo ni suala la kusubiri na kuona nini
kitatokea.
0 COMMENTS:
Post a Comment