August 24, 2019


Ni kama mtihani mzito kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kutokana na ujio wa maboresho wa kanuni mpya za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) msimu ujao.

Mtihani huo unakuja kutokana na moja ya kanuni zilizotangazwa juzi na Bodi ya Ligi (TPLB) kuwa kutakuwa na adhabu kwa kiongozi yeyote kunako benchi la ufundi la timu husika juu ya uvaaji usio na heshima.

Kanuni hii inakuwa ngumu kwa Zahera ambaye amezoea kuvaa pensi fupi anapokuwa kwenye mechi jambo ambalo linaweza kumfanya akaja na mwonekano tofauti msimu ujao.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, Zahera ameonekana kutaniwa haswa na wale mashabiki wa Simba kutokana  na aina yake ya uvaaji wakimsema kuwa anaweza kukutana na adhabu kali ikiwemo kupigwa faini.

Kanuni hiyo na nyingine mpya zitaanza rasmi ligi itakapoanza kwa msimu ujao.

1 COMMENTS:

  1. Unatakiwa kurejea kanuni za michezo na ubainishe kama pence au bukta soyo vazi la heshima

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic