September 7, 2019


Mwanachama na Mjumbe wa Baraza la Wazee katika klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali, Alhamisi ya wiki amepokea mchango wa fedha, kiasi shilingi za kitanzania 1900.

Fedha hizo zimetoka kwa baadhi ya wadau ambao wameguswa naye zikiwa ni kwa ajili ya kumsaidia kulipa deni analodaiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kutibiwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

Akilimali amesema tangu aanze kuchangiwa Jumapili iliyopita, mpaka sasa amepokea jumla ya shilingi 34,700 pekee.

Baada ya kupokea kiasi hicho cha pesa, Akilimali sasa amebakiza jumla ya shilingi 334,000 ili kulipa deni la 369,000 ambalo anadaiwa katika hospitali ya Muhimbili.

"AlhamisI hii wamenitumia 1900, ndizo fedha nilizopokea, lakini tangu waanze kunichangia nimefikisha shilingi 34,700.

"Nawaomba wadau, haswa wanachama na mashabiki wa Yanga wazidi kunisaidia kwa chochote walichonacho ili niweze kulipa deni hili, maana nisipolipa mapema, huduma ambazo naendelea kupewa Muhimbili nitasitishiwa".


1 COMMENTS:

  1. Wanayanga jaman tutoe hiyo pesa ya vitafunwa tu Mzee wetu huyu akilimali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic