September 12, 2019


Baada ya kupata taarifa za kuugua kwa Katibu wa Baraza la Wazee la Klabu ya Yanga, mzee Akilimali, timu ya Global TV Online imeamua kufunga safari mpaka nyumbani kwake kwa ajili ya kumjulia hali.

Akizungumza na Global TV nyumbani kwake,  akiwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni, ametoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliomsaidia fedha za matibabu akiwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.

“Nimeshangaa sana, kuna mtu amejifanya yeye ni ‘Ridhiwani’, akaniahidi kwamba atanitumia pesa za matibabu mpaka sasa ameingia mitini…  Kuna wengine wanatumia lugha mbaya za kunitukana kwamba nimeisha.

“Tulikuwa tukiendeshwa na Yanga kivuli kiujanjaujanja…. kwa picha ya samaki…. Tunaambiwa Manji yupo wala haonekani, lakini leo hii tuna uongozi imara, chini ya Dkt. Msolla na watendaji wengine. Hiki ndicho nilichokuwa nakitaka.

“Mimi ndiyo nimeifanya Yanga imebaki mikononi mwetu wanachama. Wanasema eti niachane na Yanga, mimi siwezi kuachana na Yanga. Nilichokuwa nikikataa ni kuikodisha Yanga kama masufuria ya shughuli,” amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic