Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Kubashiri ya Premier Bet, leo Jumanne imelitambulisha huduma zake mbili za kucheza mchezo huo huku wakiweka dau la Sh milioni 500 kwa mshindi wa Premier Bet Jackpot.
Mshindi huyo atakayeshinda mamilioni hayo ni yule atakayebashiri kwa usahihi mechi 18 huku kikiwekwa kiasi cha fedha kama kifuta jasho kwa wale watakaobashiri kutokana na idadi ya mechi walizoziweka.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Ujasiriamali Watu wa Premier Bet, Amanda Kombe alisema kuwa wamezitambulisha huduma zao mbili kwa wateja wao ambazo ni Football Jackpot King na Cash Out.
Kombe alisema kuwa wameziboresha huduma zao hizo ambazo zitapatikana kwa njia ya online kwa wateja wao wanaocheza na michezo yao ya kubashiri kupitia huduma hiyo.
Aliongeza kuwa, michezo hiyo ya kubashiri inashirikisha watu kuanzia umri wa miaka 18 watakaopata nafasi ya kucheza michezo yao ya kubashiri kwa kuanzia shilingi 200 pekee.
“Tumekuja kugawa fedha kwa Watanzania, ni rahisi tu mtu anachotakiwa ni kujisali kuingia kwenye familia ya Premier Bet kwa ajili ya kucheza michezo yetu ya kubashiri.
“Tumeweka kitita cha shilingi milioni 500 kwa Watanzania watakaoshindania Jackpot yetu hiyo kwa shilingi milioni 500, hivyo ili mshindi ajishindie fedha hizo, basi kubashiri kwa usahihi mechi 18 tutakazoweka siku ya wikiendi kuanzia Jumamosi na Jumapili.
“Pia, tofauti na Jackpot kubwa ya shilingi milioni 500, tumeweka kifuta jasho kwa washindi wengine watakaotabiri vema mechi hizo ambazo ni mechi 17 atachukua shilingi milioni 10, atakayepatia michezo 16 yeye atabeba shilingi milioni 2 huku zile 15 basi atajishindia shilingi 400, 000,” alisema Kombe.
Aidha, katika hatua nyingine Kombe aliwatambulisha mabalozi wapya wa Premier Bet ambao ni Lucas Muhavile ‘Joti’, Jacob Mbuya, James Tupatupa na Fatma Likwata.
JOIN NOW @ PREMIER BET TANZANIA
ReplyDeletehttps://bit.ly/34CiZ9w