September 11, 2019


UONGOZI wa Azam FC umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa hatua ya Kwanza wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Jumapili dhidi ya Triangel United ya Zimbabwe.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', amesema mashabiki ni muhimu kuipa sapoti timu yao ili ifanye vema kwenye michuano ya kimataifa.

"Tumejipanga kufanya vizuri na kupata matokeo chanya imani ni kwamba uwepo wa mashabiki utaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana.


"Mchezo wetu uliopita dhidi ya FC Kenema mashabiki walijitokeza wengi na timu ikapata matokeo na inawekezekana kwani tupo vizuri," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic