September 11, 2019


Mchezo wa kirafiki uliozikutanisha timu za Waliooa FC na Wasiooa FC kutoka katika Kampuni ya Global Group, ulifanyika Ijumaa iliyopita kwenye Uwanja wa CCM, Sinza jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa na kila aina ya burudani, ulimalizika kwa Waliooa FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Waliofanikisha kwa kiasi kikubwa kuchezwa kwa mchezo huo ni Salehjembe Blog na Shavilla Hotel waliyoidhamini timu ya Waliooa FC pamoja na Kessy Marketing Agency na Ashishi Cinematographer ambao waliidhamini timu ya Wasiooa FC.

Akizungumzia udhamini wao, Nahodha wa Waliooa FC, Phillip Nkini, alisema: “Kiukweli haikuwa rahisi mpaka mchezo huu kuchezwa, niseme tu, kwa upande wetu tunaishukuru Salehjembe Blog na Shavilla Hotel iliyopo Tegeta Namanga kwa udhamini wao kwetu, lakini pia viongozi wa timu ya Sinza Boys kwa kutupatia uwanja ambao tuliutumia kuchezea mechi ile.”

Naye Nahodha wa Wasiooa FC, Omary Mdose, alisema: “Unajua siku zote jambo lako ukitaka ulifanikishe kwa kiasi kikubwa ni vema ukashirikiana na wenzako, hivyo basi hatuna budi kuwashukuru washirika wetu ambao walitushika mkono mwanzo hadi mwisho wa mechi hii.

“Udhamini mnono tulioupata kutoka Kessy Marketing Agency na Ashishi Cinematographer ulitusaidia sana hadi tukacheza mechi kwa amani na utulivu wa hali ya juu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic