September 2, 2019


Dondoo za mkutano wa jana Baina ya Matawi na Mwenyekiti wa klabu Mshindo Msolla

Mkutano ulikua na lengo moja kuhamasisha amani na umoja ndani ya Yanga kuelekea mechi na Zesco pamoja na mechi 37 za ligi kuu zilizobaki

Matawi yasaidiane pamoja na klabu kuhakikisha Yanga inashinda mechi zake zote zilizobaki za ligi kuu pamoja na mechi ya Kimataifa

Katika kuleta umoja wa klabu tuondoe makundi makundi yote yaliyokuwepo Wakati wa uchaguzi na Sasa Yanga iwe moja atakayechochea makundi kupelekwa Kamati ya Nidhamu kushugulikiwa

Matawi yafanye chaguzi kufikia December na katika kuhakikisha Hilo litasimamiwa Mwenyekiti yupo mbioni kuunda Kamati ya Matawi na wanachama itakayokua inasimamia Masuala ya Matawi na wanachama kwa ujumla.

-Kwa muda wa miezi minne Kamati mpya ya Utendaji imekwisha ingia mikataba  zaidi ya minne kuhakikisha Yanga inakua vyema kiuchumi

-Jengo la klabu Yetu Sasa ukarabati utaanza muda sio mrefu na utafanywa na Kampuni ya GSM kwa kua moja ya masharti katika tender ya jezi iwaliyopewa limo pia sharti la kukarabati Jengo ili Sasa Tupunguze matumizi ya kukaa hotelini,ukarabati  utahusisha pia sehemu ya mazoezi ya viungo Gym pamoja na bwawa la kuogelea lililopo katika Jengo letu.

Mpaka Sasa Yanga Ina mkataba na Sportpesa ambao mwaka huu watatoa Bilioni Moja na milioni 94,Uongozi umefanikiwa kupataa mikataba na Taifa Gas toka kwa Rostam ambao watato milioni 300 lakini pia ushirikiano na Mh Rostam bado upo ndie aliyetoa milioni 60 kuvunja mkataba wa Kindoki na pesa za kumleta Molinga Yanga,Mkataba na GSM wa Kwanza  ni ule wa jezi ambao klabu unapata TSH 1300 kwa kila jezi itakayouzwa na lengo ni kuhakikisha jezi milioni 1 zinauzwa ili klabu ipate Bilioni Moja na milioni 300 ,pia mkataba unahusisha ukarabati wa Jengo la Yanga,Mkataba wa pili na GSM unahusisha magodoro ya GSM mkataba huu una thamani ya milioni 150, Klabu ipo mbioni kuongeza mdhamini mwingine toka Kampuni ya Vinywaji atakayetoa pesa Kama ilivyo Sportpesa na pia kukarabati pitch ya uwanja wa Kaunda uwe wa kisasa kutumika katika mazoezi ndio maana zoezi la kuweka kifusi linaendelea kwa kasi.

Si kweli kwamba Mwl Zahera amepewa siku Tatu Bali juzi Kulikua na kikao cha Kamati ya Utendaji na kocha aliitwa atambulishwe rasmi kwa wajumbe na pia ashauri mikakati ya kuelekea mechi na Zesco na kiujumla Uongozi una imani na kocha na wanaushirikiano mzuri  hivyo habari kua amepewa mechi tatu tuzipuuze.

Kuhusu sectretaliet tayari mchakato wa kuwapata Katibu na wakurugenzi wa idara mbalimbali Kama Fedha ,Masoko,Ufundi na Mashindano umeshakamilika na wiki hii watapewa ofa ya mikataba tayari kwa kuanza kazi

Timu itaelekea Mwanza kwa maandalizi ya mechi na Zesco itaondoka Tarehe 4 Mpaka tarehe 11 Itakua Mwanza ,ikiwa Mwanza kutakua na Kubwa Kuliko tamasha la kuichangia Yanga lililoandaliwa na wanayanga wenyewe wa Mwanza,wana Mwanza wamelipia kila kitu kuhusu safari hiyo hivyo klabu haitahusika na gharama yeyote na itafaidika katika mechi 2 za kirafiki kwa kupata 85% ya gate collection.

Gazeti la Yanga liko mbioni na litalejea mda sio mrefu

Mwisho wanayanga wote tusameheane wale waliokua nje ya Timu na sasa wamerudi Ni juhudi za Mwenyekiti kuhakikisha Yanga yote tunakua wamoja hivyo tusijenge visasi tunapowaona tushirikiane nao kuhakikisha Yanga inakua moja.

Kila mwanachama asiache kuhudhuria mechi yetu na Zesco.

Katibu Tawi VIVA


3 COMMENTS:

  1. Uongozk ukifanikiwa issue ya ukarabati wa jengo pamoja na uwanja wa mazoezi kaunda wachezaji wakawa wanatokea klabuni wanashuka tu ngazi kuelekea mazoezini hakika historia itawakumbuka

    ReplyDelete
  2. Ningependa kutoa ushauri ufuatao:

    1. Kufanya UHARAKA katika utekelezaji wa mambo mengi mfano UKARABATI NA UJENZI WA JENGO LA KLABU NA UWANJA WA MAZOEZI....KUMEKUWA NA AHADI NA UZITO WA KUFANYA UJENZI....

    2. KUFANYA HARAKA UJENZI WA MRADI WA KIGAMBONI YANGA COMPLEX....KUMEKUWA NA UZITO NA KUSUASUA

    3. Uhamasishaji kuelekea mechi ya tarehe 14 uanze sasa hivi...kumekuwa na siasa na ahadi bila ya vitendo

    4. Uingizaji ama uandikishaji wa wanachama na wapenzi wapya wa Yanga nchi nzima umebaki kuwa mipango tu hakuna utekelezaji

    5. Kubadilishwa kwa mfumo wa uendeshaji kutoka umiliki wa 100% kwa wanachama na kuingia soko la hisa (51% wanachama , 49% wawekezaji wasiopungua 3)...utekelezaji umekuwa mdogo ama unasuasua au hautangazwi kuujulisha umma ulipofikia na kwanini auendelei?

    Ahsante

    ReplyDelete
  3. Huwezi ukawa na mipango hiyo yote kwa wakati mmoja wakati timu hapo kabla ilisua sua kwa kukosa pesa acheni kushindana kijinga viongozi wa yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic