September 12, 2019


Na George Mganga

Aliyekuwa straika wa Yanga, Mrundi, Amis Tambwe, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumpa mkataba Kocha Ettiene Ndayiragije wa kuinoa Taifa Stars.

Tambwe ambaye hivi karibuni amesajiliwa na Fanja FC ya Oman huko Uarabuni, anaamini kwa namna ambavyo Stars inavyocheza soka chini ya Ndayiragije ambaye ni raia wa Burundi, ni wakati mwafaka wa yeye kupewa mkataba.

Tambwe amesema kitendo cha Ndayiragije kuisaidia Stars kuingia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022, Qatar, ni sifa tosha kwake kumwaga wino.

"Ninaona ni wakati mwafaka kwa Ndayiragije kupewa mkataba na TFF kwani ameifanya Stars icheze soka la zuri.

"Ujue siku zote huwa tunaangalia kocha anayepata matokeo, kama timu bado ipo kwenye nafasi ya kuwania nafasi ya kufuzu kwenda CHAN pamoja na Kombe la Dunia, kwa nini asipewe mkataba?

"Hamna haja ya kupepesa macho katika hilo, ni wakati mwafaka kwake kupewa timu na naamini ataisaidia kufika mbali kwa namna alivyosuka akiwa na muda mfupi," amesema Tambwe.

Ndayiragije amefanikisha kuipeleka Stars katika hatua ya makundi kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuiondoa Burundi Jumapili iliyopita kwa ushindi mabao 3-0 uliopatikana kwa njia ya matuta kufuatia dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1.

3 COMMENTS:

  1. Mbona Viongozi wa kuchaguliwa wa Timu ya Wananchi hamuweki Press Conference kwa ajili ya masuala yafuatayo???
    1. Hamasa mechi na Zesco
    2. Kutambulisha Secretariat mpya
    3. Kutangaza maendeleo ya miradi mbalimbali (Ujenzi wa Uwanja, ukarabati wa jengo la klabu)
    4. Kutangaza udhamini uliongia na kiasi gani klabu inapata
    5. Kutangaza mipango ambayo ipo mbioni na ambayo tayari imeshatekelezwa

    MSIWE BARIDIIIIIII!!!!!!!
    Ahsante....

    ReplyDelete
  2. Eti wapi katika dunia ya leo mtu au timu itatangaza waziwazi jinsi atakavyo pambana na adui au timu pinzani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic