September 22, 2019


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameamua kuomba kipindi Azam ili kuchuana na Mwanahabari mwenzake aliyeteuliwa siku kadhaa zilizopita, Hassan Bumbuli.

Bumbuli hivi karibuni alitangazwa na uongozi wa Yanga kuchukua nafasi ya Dismas Ten aliyekuwa Msemaji wa klabu hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara aliandika akiomba awekwe pamoja na Bumbuli ili wazungumzie mambo ya Professionalism.

Kauli hiyo ilikuja kufuatia Bumbuli kumsema Manara kuwa amekuwa ni mtu wa propaganda tofauti na kufanya kazi kwa ueledi.

Manara alionekana kuchukizwa na kauli ya Bumbuli ambayo imezua gumzo kubwa jana mpaka kupelekea Manara kuanza kumjibu kwenye mitandao ya kijamii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic