SELEMAN
Matola, Kaimu Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa
mashabiki wanapaswa waendelee kuipa sapoti timu yao bila kuchoka.
Stars
imefanikiwa kutinga hatua ya Makundi kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar
baada ya kupata ushindi wa penalti 3-0 mbele ya Burundi kutokana na kutoshana
nguvu kwenye michezo yote miwili.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burudi matokeo yalikuwa ni 1-1 sawa na ule wa marudio uliopigwa Dar na ulipelekea kuongezwa dakika 30 ila matokeo hayakubadilika.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa nguvu ya mashabiki ina matokeo chanya na
uwepo wao uwanjani una nguvu.
“Tunaona
wachezaji wanfurahi kuona uwepo wa mashabiki uwanjani, pia kila mmoja anapenda
kuona timu inapata matokeo hivyo sapoti ni muhimu.
“Kwa sasa
mashabiki wanapaswa waendelee kutoa sapoti kuwani inawapa hamasa wachezaji kufanya
vizuri, ni jambo la kupongezwa kwa mashabiki kuwa na uzalendo,” amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment