NYOTA wa
timu ya Simba, Ibrahim Ajibu ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili
kuitumikia timu hiyo akitokea Yanga amesema kuwa maajabu yake yanaanza kuonekana
kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar.
Simba
itamenyana na Mtibwa Sugar, kesho uwanja wa Uhuru
baada ya ratiba kubadilishwa kwani awali mchezo ulipangwa kuwa Septemba 18.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ajibu ambaye msimu
uliopita akiwa ndani ya Yanga alitoa assisti 17 na kufunga mabao
sita amesema kuwa Simba watampenda.
“Nimeanza maisha
mapya sehemu nyingine tofauti na msimu uliopita sasa hesabu zangu ni kufanya
vizuri kwa manufaa ya timu kwani timu inapofanya usajili inakuwa na malengo na
mchezaji nami nina malengo yangu.
“Michezo
yote kwangu ni muhimu hata unaofuata ambao ni dhidi ya Mtibwa tunataka kufanya
vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kwa sasa kazi inaanza na
tutapambana kwa ajili ya timu mashabiki watupe sapoti,” amesema Ajibu.
Mchezo wa
kwanza Ajibu kutumikia akiwa ndani ya Simba ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania uwanja
wa Uhuru alicheza kwa dakika 13 baada ya kuingia dakika ya 77 akichukua nafasi
ya Clatous Chama, Simba ilishinda mabao 3-1.
Pamjaa xan kamanda
ReplyDelete