LEICESTER City leo wameinyoosha timu ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kwa Ushindi wa mabao 2-1.
Mabao ya Leicester yamefungwa na Ricardo Domingo's Barboss Pereira dakika ya 69 na la ushindi likifungwa na James Madison dakika ya 85.
Bao la Kwanza Kwa Tottenham Hotspur lilipachikwa na Harry Kane dakika ya 29.
Mchezo huu uliopigwa Uwanja wa King Power ulikuwa ni wa kukata na shoka uliongozwa na refarii Paul Tierney.
Dakika ya 15 Leicester City walipachika bao kupitia Kwa Ndindi aliyemalizia mpira wa kona iliyokuwa inazagaa langoni ikamshinda mlinda mlango Ila bao hilo likakataliwa na VAR kwa kuwa walikuwa wameotea.
Mchezo wa leo ulimshuhudia nyota Wanyama akiingia dakika ya 69 akichukua nafasi ya Sissoko.
Mabadiliko hayo hayajafuta rekodi ya Spurs kushindwa kupata ushindi ugenini tangu January 20.
0 COMMENTS:
Post a Comment