KOCHA Mkuu
wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa ataona fahari wachezaji wake ambao
wameitwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania endapo watafanya kweli
kwa ajili ya Taifa.
Nyota mpya
wa Simba, Miraj Athuman’Sheva’ amekuwa shujaa ndani ya dakika 180 jambo
linalofanya ujumbe huu kumhusu jumla anapoingia kwenye majukumu ya Taifa.
Stars kesho
itamenyana na Sudan kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Chan
inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon mwaka 2020.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa anaona fahari wachezaji wake
wanapoitumikia timu ya Taifa kwani ni majukumu makubwa na yenye manufaa.
“Napenda
kuona wachezaji wakifanya vizuri pindi wanapokuwa kwenye timu ya Taifa,
nitapenda kuona kile ambacho wanakifanya wakiwa na timu wanafanya tena kwenye
timu ya Taifa,” amesema Aussems.
Wachezaji wa
Simba ambao wameitwa kikosi cha timu ya Taifa ni pamoja na Haruna Shamte,
Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin,
Hassan Dilunga na Miraj Athuman ‘Sheva’.
0 COMMENTS:
Post a Comment