September 13, 2019





FULL TIME: SIMBA SC 2-1 MTIBWA SUGAR

Dak ya 90+3, kadi ya njano inakwenda kwa Salum Kanoni, dakika za jioni kabisa.
Dakika zimeongezwa tatu kumaliza mpira, zimesalia mbili sasa.

Dak ya 90, Jonas Mkude anaingia kuchukua nafasi ya Shiboub
Dak ya 81, Imepigwa faulo ile kwake Kahata inamkuta na anajaribu kumalizia lakini mpira unamzidi kasi, golikiki.
Dak ya 81, Mtibwa wanacheza faulo, inapigwa kuelekezwa langoni kwao, nafasi ya Simba kupata bao la tatu.
Dak ya 79, Kahata anaingia kuchukua nafasi ya Chama.
Dak ya 77, Kona nyingine kwa Simba, ni baada ya Kapombe kubabatizana na Kapombe. Inapigwa lakini inakuwa golikiki.

Dak ya 74, Simba wanaanza tena upya, Yassin kwake Athuman, piga kwake Kado anadaka mpira.
Dak 68, Mirajiiiiii, anaifungia Simba bao la pili kwa shuti kali akitoka kupokea pasi nzuri kutoka kwa Shiboub
Dak ya 67, Mtibwa wanaonesha jitihada za kulinda zaidi eneo lao na wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa Simba.
Dak ya 63, Simba wamefanya shambulizi la kutisha langoni mwa Mtibwa lakini mawasiliano yamekuwa si mazuri na Mtibwa wanaokoa.

Dak ya 62, Miraji Athuman anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga.
Dak ya 60, Simba wameanza tena, Chama anachukua, anampasia Nyoni, wanajaribu kupenya ngome ya Mtibwa, kwake Kagere lakini Mtibwa wanawadhibiti.
Dak ya 57, Tayari Kado ameshasimama na mpira umeshaanza, Simba wanaanza kwa kupasiana vema langoni mwa Mtibwa, unamkuta kwake Chama, anapiga shuti ambalo linapaa nje ya lango.

Dak ya 55, Mpira umesimama, Kado ameumia, Kahata naye anaonekana kama anataka kuchukua nafasi ya mtu.
Dak ya 52, Kado anaokoa nafasi nyingine kutoka kwa Yassin aliyepata nafasi ya kufunga, kama angekuwa dhaifu angeshafungwa zaidi ya bao mbili.
Dak ya 52, Kagere anaotea, anaonekana kulalamika kwa kuonesha ana njaa ya kufunga.
Dak ya 49, Aishi Manula anaanzisha upya mashambulizi, ni kipindi cha pili sasa.

MAPUMZIKO: SIMBA SC 1-1 MTIBWA SUGAR

Dak ya 47, Chama amepiga lakini inakwenda nje.
Dak ya 46, Humud anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi, ni ya kwanza ndani ya dakika 45 za kwanza, ni faulo.

Dak ya 44, Fraga anababatizana na mchezaji wa Mtibwa, mpira unakwena nje, unarushwa kuelekea Mtibwa.
Dak ya 42, Tayari Shiboub alishaamka, na zikiwa zimesalia dakika mbili mpira kwenda mapumziko.
Dak ya 41, Shiboub anafanyiwa madhambi, na mpira umesimama kwa muda.
Dak ya 38, Kanoni anatolewa nje na machela baada ya kuumia, matokeo bado ni 1-1.
Dak ya 37, Chamaaaaa, pata nafasi moja maridadi kabisa lakini shuti lake linakwenda moja kwa moja kwa Kado kwa kulidaka.

Dak ya 33, Inapigwa lakini inakwenda moja kwa moja kwa Manula ambaye anapangua na kuuelekeza eneo la kati mwa uwanja.
Dak ya 32, Mtibwa wanapata faulo, anakwenda kupiga Salum Kanoni, piga mkwaju mkali unapanguliwa na Manula, inakuwa kona.
Dak ya 31, Mtibwa wanajichanganya eneo lao la ulinzi, Simba wanaudaka kwake Kagere, bahati si yake. Kipa anadaka.
Dak ya 30, ni kona nyingine inapigwa kuelekezwa Mtibwa, anapiga Chama, piga kule lakini inababatizwa na wachezaji wa Simba, golikiki.
Dak ya 28, Mpira umesimama kwa muda, mchezaji wa Mtibwa ameumia.
Dak ya 27, Offside kwa, mpira unachezwa na Mtibwa.

Dak ya 25, Kapombe anapasiana na Chama eneo la kati mwa Uwanja, maelewano yanakuwa si mazuri, na mpira unakuwa golikiki, unaelekezwa Simba.
Dak ya 24, Mpira unarushwa kuelekea lango la Mtibwa, ni karibu na eneo la kona, umesharushwa na unatolewa tena.
Dak ya 21, Rifat Hamis anaisawazishia Mtibw aSugar kwa mpira wa kichwa ulitokana na kona, ni 1-1.
Dak ya 17, Goooli, Meddie Kagere anafunga bao la kwanza baada ya Simba kupasiana vema katika eneo la hatari, sasa ni 1-0.

Dak ya 10, Golikiki imetokea upande wa Simba, wanaanza upya kwake Manula.
Dak ya 9, Simba wanapata kona ya kwanza,wanapiga lakini inatolewa nje na Mtibwa, wanaenda kurusha, Chama anarusha.
Dak ya 7, Simba wanatandaza pasi nzuri kuelekea Mtibwa, kwake Shomari Kapombe, anapiga krosi ambayo inashindwa kuzaa matunda.
Dak ya 6, Kado anaokoa mpira uliopigwa na Chama akiwa peke yake, ni nafasi ambayo Simba wamngeshaandika bao.
Dak ya 6, Bado Simba wanaonekana kuutawala mchezo zaidi ya Mtibwa kwa dakika hizi sita za mwanzo.

Dak ya 4, Simba wanaanza faulo kwa kupasiana, anapiga Nyonii, inaokolewa na mabeki wa Mtibwa.
Dak ya 3, Zimbwe Jr anakokotoa mpira na guu la kushoto kushoto mwa uwanja, mchezaji Awadhi Salum wa Mtibwa anashikana mkono, faulo.
Dak ya 3, Manula anadaka mpira, anaanzisha mashambulizi upya.
Dak ya 2, Rifat Hamis wa Mtibwa anapandisha mashambulizi kwenda Simba, ni la kwanza.
Dak ya 1, mechi imeshaanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, na Simba wameanza kwa kushambulia kwa kasi lango la Mtibwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic