LWANDAMINA AWACHOKOZA YANGA
Kocha wa zamani wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina amefunguka kuwa anakuja Tanzania kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anaifunga timu hiyo katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabigwa Afrika.
Lwandamina ambaye kwa sasa amerejea kwenye timu yake ya zamani, Zesco United, baada ya kuachana na Yanga msimu uliopita kabla ya kutua Mwinyi Zahera raia wa DR Congo.
Mzambia huyo anatarajia kukutana na timu yake hiyo ya zamani katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kati ya Septemba 13-15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Septemba 27, mwaka huu nchini Zambia.
Lwandamina anakutana na Yanga kwenye hatua hiyo baada ya kuwaondoa Green Mamba huku Yanga ikiwaondoa mabingwa wa Ligi Kuu ya Botswana, Township Rollers.
Lwandamina alisema kuwa anakuja nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anaifunga Yanga katika mchezo wa hatua ya kwanza kabla ya mchezo wa marudiano utakaonfanyika kwao Zambia.
“Unajua timu yeyote kwenye michuano hii inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele na ndivyo ilivyo kwetu, ninakuja Tanzania kwa mara nyingine lakini kwa sasa ninakuja kwa ajili ya kazi moja tu ya kuhakikisha ninaifunga Yanga.
“Yanga ni timu nzuri na kwa sasa ina wachezaji wengi wageni ambao sikuwahi kuwafundisha, pia huwezi kuwalinganisha wachezaji hao wapya na wachezaji ambao walikuwepo wakati niko Yanga kwa sababu wana tofauti kubwa, lakini kama nilivyosema awali kwamba waambie Watanzania, Lwandamina anakuja kuifunga Yanga,” alisema Lwandamina.
0 COMMENTS:
Post a Comment