LICHA ya kutangulia kufunga bao dakika ya 10 leo mbele ya Southampton kupitia kwa Daniel James bado wamekwama kusepa na pointi tatu muhimu.
Dakika ya 58 Southampton walichomoa bao hilo kupitia kwa Jannik Vestergaad na kuwafanya Unted wakubali kugawana pointi mojamoja leo.
Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkali ambapo imeshuhudiwa kadi nyekundu ikitolewa kwa Kevin Danso wa Southampton dk ya 73.
Huu ni mchezo wa pili United kulazimisha sare katika michezo minne waliyocheza, wameshinda mchezo mmoja pekee mbele ya Chelsea na wamepoteza mchezo mmoja mbele ya Craystal Palace.
0 COMMENTS:
Post a Comment