September 1, 2019


Na George Mganga

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Alliance Shools ya Mwanza, Athuman Bilali Bilo, amesema kuwa alifukuzwa kwa sababu ya kuingiliwa majukumu yake kwenye benchi la ufundi na Mkurungezi wa timu hiyo, James Bwire.

Bilo amefunguka kuwa alikuwa alishinikizwa kupanga kikosi na bosi wake jambo ambalo lilikuwa likimkwaza na kupelekea ugomvi ambao ulisababisha atimuliwe.

Kocha huyo amesema Bwire alikuwa akimpangia hata wachezaji anaopaswa kuwafanyia mabadiliko wakati wa mechi sababu Bwire amekuwa na tabia ya kukaa kwenye benchi la ufundi.

"Pale Alliance kuna matatizo makubwa mno, bosi wangu amekuwa akinipangia kikosi mpaka SUB, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za majukumu ya Kocha.

"Si mimi tu, hata Mbwana Makata na Malale Hamsini walikuwa wakikutana na changamoto kama hizo wakati wanaifundisha timu hiyo, inasikitisha.

"Kiukweli mimi ilifikia wakati nikaona uvumilivu umenishinda na mpaka tulivurugana mwisho wa siku nikafutwa kazi.'

Bilo ameeleza kuwa kwa sasa hana kazi na hajafanya mazungumzo na timu yoyote hivyo anazikaribisha klabu ambazo zinahitaji huduma yake kukaa mezani ili wazungumze.

Ikumbukwe kabla Bilo hajajiunga na Alliance, Kocha huyo alikuwa anaifundisha Stand United ya Shinyanga iliyoshuka daraja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic