MATAJIRI YANGA KUFURU MWANZA
KUFURU tupu Yanga! Ndivyo unaweza kusema baada ya matajiri wa timu hiyo kutoa ahadi za uendelea kuisaidia klabu hiyo huku Kampuni ya GSM ikiingia mkataba mpya utakaoifanya Yanga kupata Sh mil 50.
Shangwe hilo lilitokea kuanzia mida ya jioni jijini hapa ambapo Yanga ilikuwa inafanya kongamano maalumu la kuichangia timu hiyo kwenye Ukumbi wa Maduhu Square jijini hapa.
Katika harambee hiyo ambayo ilihudhuriwa na wanachama zaidi ya 400 mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliyetakiwa kuwa mgeni awali.
MSOLLA AFUNGUA NJIA
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alikuwa kiongozi wa kwanza kwa upande wa klabu hiyo kuingia ukumbini hapo majira ya saa 11:40 jioni ambapo alipokelewa kwa shangwe kubwa na wanachama ambao waliojitokeza kwa wingi ukumbini hapo.
Kabla hakujatulia vizuri akatokezea bilionea ambaye amekuwa akiifanya Yanga iishi kifalme inapokwenda Mwanza, Yanga Makaga ambaye naye alipata mapokezi ya aina yake kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo.
Moja kwa moja Makaga ambaye alikuwa ametinga uzi wa kijani wa klabu hiyo alikwenda kukaa meza moja na Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten ambapo walionekana wakibadilishana mawazo mara kadhaa.
Wakati wanachama wakiendelea ‘kushangweka’ akafi ka mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Dk Philis ambaye alipokelewa na Msolla na moja kwa moja akaenda kukaa naye meza kuu kusubiri tukio lianze.
Akizungumza mbele ya wanachama, Msolla alianza kwa kuwaomba radhi mashabiki kutokana na kuzalisha jezi chache na kwamba leo Jumamosi Kampuni ya GSM ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo itashusha jezi milioni moja zitakazotua nchini na Yanga itapata gawio la Sh bil1.3 kwa kuwa kila jezi Sh 1300 itaingia Yanga.
Msolla aliongeza kuwa, wameingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya GSM ambao utaifanya Yanga kupata Sh mil 50 ambapo kampuni hiyo itatengeneza khanga.
Aliongeza kuwa, mkataba huo unaweza kuongezwa ikiwa biashara hiyo itaenda vizuri na hivyo kuipa Yanga fedha ambazo zitasaidia kwenye vitu mbalimbali.
“Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na GSM kwa ajili ya kutengeneza khanga za Yanga na sisi kama klabu tutanufaika kwa kupewa Sh mil 50.
“Mkataba unaweza kuboreshwa zaidi ikiwa biashara itakavyokuwa nzuri,” alisema Msolla na kuwaamsha wanachama waliokuwa wamekaa kimya wakimsikiliza.
Aidha Msolla ambaye ameingia madarakani mwaka huu alisema hadi kufi kia Desemba mwaka huu klabu hiyo anataka iwe na wanachama milioni moja tofauti na sasa ambapo wapo 14,000 wanaotambulika nchini nzima kwa kulipa ada.
BILIONEA AAHIDI USHINDI UHAKIKA
Bilionea anayejitoaga sana kwa Yanga inapokuwa Kanda ya Ziwa, Makaga ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu na wanachama wa klabu hiyo kusikia ahadi yake alipopewa nafasi alisema kwa kifupi tu:
“Ninaahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa kamati ya roho mbaya kuhakikisha Yanga inashinda katika mchezo dhidi ya Zesco.”
Pia bilionea huyo katika harambee hiyo alitoa kiasi cha milioni mbili kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo.
ZAHERA HAYUPO NYUMA, ATOA MILIONI
Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera naye kwa kuonyesha kwamba hayupo nyuma jana alitoa milioni moja kwa ajili ya klabu yake hiyo.
Huu ni muendelezo kwa kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa kutoa fedha zake za mfukoni kwani kwa msimu uliopita alikuwa akijitolea kwenye mambo mbalimbali.
Ongea juu ya ushindi unaotakiwa na usiongee kufuru za matajiri. Mashabiki wanataka ushindi sio kufungwa na vitimu dhaifu kila kukicha bwana.
ReplyDeletehii ni mara ya ngapi hii habari kuchapishwa?
ReplyDeletehizi habari ndio zinazo ichimbia yanga kabuli
ReplyDeleteKwa maana nyingine huyu mwandishi ni wa upande mwingine kabisaa maana sijaona mamilioni unayoyataja unadharau na wala huna uwadilifu kwenye uwandishi wako
DeleteHuenda huyu muandishi analipwa chochote kutamka hata mabilioni Kwa sababu mbili, moja kuwafanya mashabiki wasaha vipigo vya marakwamara na kuwafanya mastaa WA timu nyengine watake kujiunga nao na wale waliokuwa mguu nje na mguu ndani mguu WA nje waurudishe ndani Kwa tamaa ya kunona lakini wengi wajiuliza mbona madeni bado yanawaandama na bakuli ndio linazidi kasi. Mbona Kwa upande WA mnyama na na wana lambalamba kwenye chimbuko la hela. ya kweli hstusikii maporojo kama hayo
ReplyDelete