JUMA Kaseja mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa kinachomfanya awe bora siku zote ni kipaji alichopewa na Mungu.
Jana Kaseja aliibuka shujaa baada ya kuokoa penalti moja kwenye mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022 dhidi ya Burundi uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Stars ilipenya hatua ya makundi kwa ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 120 kukamilka kwa timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
"Nimecheza ligi kwa muda wa zaidi ya miaka 19 na hakuna mwalimu ambaye amewahi kunifundisha kudaka penalti zaidi ya kipaji nilichopewa na Mungu, sina kingine cha kusema zaidi ya kushukuru sapoti na kufanya makubwa kwa ajili ya Taifa letu," amesema Kaseja.
Mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Burundi timu zote zilitoshana kwa kufungana bao 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment