UONGOZI wa Mtibwa
Sugar umesema kuwa hauna mashaka na wapinzani wao Simba kwani wanawatambua vema
watakula nao sahani moja leo kwa kusepa na pointi tatu muhimu.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa
wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba hawana presha ya kuwakabili kwani walipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli.
“Linapokuja
suala la kuikabili timu ndani ya ligi, hakuna utofauti mkubwa kwa kuwa wote
tunawachezaji 11 uwanjani na mbinu ndizo zitakazotubeba, tunahitaji kupata
ushindi mapema tukiwa ugenini hatuna presha yoyote.
“Mpira ni
mchezo wa makosa na kinachobeba ushindi wa timu ni maadalizi kwa namna
tulivyojipanga hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuhitaji pointi tatu
muhimu,” amesema Katwila.
Mtibwa Sugar
itawakosa nyota wake watatu ambao ni Shaban Nditi, Salum Kihimbwa pamoja na
Saley Hamis kutokana na kusumbuliwa na majeruhi msimu huu huku Simba ikiwakosa John Bocco na Mbrazil Wilker da Silver.
0 COMMENTS:
Post a Comment