September 13, 2019


Nahodha wa Simba, John Bocco, amewa angukia wapinzani wao, Yanga kwa kuwaambia wafanye kweli kimataifa ili watoe nafasi kwa Tanzania kuingia timu nne.

Nahodha huyo amesema hayo ikiwa kesho Jumamosi, Yanga wanatarajiwa kushuka uwanjani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Bocco ameliambia Championi Ijumaa, kuwa ni lazima Yanga wafanye vizuri kwenye mechi yao
hiyo na kufika mbali ili kuifanya Tanzania ipate nafasi ya kuingiza timu nne.

“Ni lazima Yanga wapambane kwenye mechi hii ya Ligi ya Mabingwa kwani kwa kufanya kwao vizuri kutatupa tena nafasi Tanzania kuingiza timu nne katika michuano hii.

“Uwezo wa kuwafunga Zesco wanao ila kitu kikubwa ni kwamba wanatakiwa wapambane vilivyo kuona wanashinda katika uwanja wa nyumbani.

“Ni mechi muhimu kwa pande zote mbili ila niwaambie tu kwamba wanachotakiwa kupambana kwani kila kitu kinawezekana wakiamua kupambana,” alisema Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic