UONGOZI wa
Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa hesabu zoa kubwa ni kupata pointi tatu
muhimu mbele ya Simba mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 17 uwanja wa Uhuru.
Mtibwa Sugar
walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Lipuli FC
itamenyana na Simba ambayo ilishinda mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania uwanja wa
Uhuru.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa
wanawaheshimu wapinzani wao Simba ila wanachohitaji ni pointi tatu.
“Mchezo wa
kwanza tulipoteza mbele ya Lipuli sasa ni muhimu kwetu kushinda mchezo wetu wa
Simba tunahitaji kupata pointi tatu zao ili kujiweka kwenye mazingira ya
ushindani.
“Kushindana
na timu bora ni jadi yetu kwani nasi tuna kikosi bora chenye uwezo wa kupambana
mashabiki watupe sapoti ya kutosha kupata burudani,” amesema Kifaru.
Si mngeliifunga Lipuli kwanza
ReplyDeletemmejipa kazi ngumu mtusamehe tafuteni baadae point tatu au subirini ile timu yenu maana na sisi tunajua mbeleni tunawababe wetu
ReplyDelete