ABDALAH Panzi ‘Dulla Mbabe’ bingwa wa ubingwa wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa
Duniani (WBO) Asia Pacific uzito wa kati (Super Middle) ambao aliupata hivi
karibuni kwa kumtwanga Zulipikaer Maimaitiali raia wa China amesema kuwa kwa
sasa atamchapa kila anayekuja mbele yake.
Ushindi huo ambao umempa heshima Mbabe ulimpa fursa ya
kupeleka mkanda huo bungeni aliupata kwa kumnyoosha mpinzani wake kwa TKO raundi ya tatu umeipandisha chati Tanzania kwa upande wa ngumi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mbabe amesema kuwa ana
imani na kile ambacho anakifanya kutokana na maandalizi ambayo anayafanya jambo
linalompa matumaini kuwafundisha adabu mabondia watakaohitaji kupambana naye.
"Mchina amenijengea uwezo wa kujiamini na kunifanya nione kwamba ninaweza kupambana na yoyote atakayetaka pambano nami hivyo sitakuwa na huruma nitamchapa kila ajaye kwangu," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment