September 11, 2019


BEKI wa Bayern Munich, Jerome Boateng mwenye umri wa miaka 31 ameshtakiwa kwa kosa la kumshambulia mpenzi wake wa zamani kwa makonde.

Ofisi ya waendesha mashtaka imepokea mashtaka dhidi ya Jerome Boateng kwa shambulio hatari alilolifanya tangu mwaka 2018.

Kufuatia Uchunguzi wa kina mashtaka yaliletwa Februari 11, 2019 alisema mwendesha Mashtaka Mkuu, Anne Leiding akithibitisha taarifa iliyovujishwa na magazeti ya Ujerumani.

Inaelezwa kuwa mpenzi wake huyo amepewa jina la herufi 'S' alikuwa ni mpenzi wake kwa muda wa miaka 10 na ni mama watoto wawili kati ya watatu wa Boateng.

Boateng ni miongoni mwa wachezaji wakubwa Ujerumani ameshinda Kombe la Dunia mwaka 2014 na Ligi ya Mabingwa Ulaya 2013.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic