MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mshambuliaji wake Sadney Urikhob anashindwa kujiamini jambo linalomfanya ashindwe kufunga mabao.
Urikhob ameshindwa kufunga kwenye michezo miwili ya kirafiki kuanzia ule wa Pamba pamoja na Toto African wakiwa Mwanza.
Michezo hii ni maalumu kwa ajili ya maadalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Zesco utakaopigwa Uwanja wa Taifa Jumamosi.
"Tatizo la Sadney pamoja na wachezaji wengine wana hali ya woga kwa sababu wanakosa sana nafasi za kufunga hili ndilo tatizo la wachezaji wangu," amesema.








0 COMMENTS:
Post a Comment