NAMUNGO FC, iliyo chini ya Hitimana Thiery leo ina kazi ya kibarua cha kulinda ama kupoteza
rekodi iliyoanza nayo msimu huu kwenye ligi kuu ambapo itamenyana na Mwadui FC ya
Shinyanga iliyo chini ya Khalid Adam.
Namungo ambayo
imepanda daraja msimu huu haijapoteza michezo miwili ya mwanzo iliyocheza
uwanja wake wa Majaliwa jambo ambalo linamuumiza kichwa Thiery kuiendelea
kuilinda.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa anajitahidi kutumia vema uwanja wa
nyumbani ili akianza safari za kutoka kikosi kiwe kimejijengea hali ya
kujiamini.
“Tuna kazi
kubwa ya kufanya kulinda rekodi yetu hii inatokana na ligi ambayo tunashiriki
kuwa na ushindani, kila kitu kipo sawa na tunajivunia kucheza nyumbani kwa kuwa
tupo na mashabiki na morali ni kubwa,” amesema Thiery.
Mbali na
Namungo leo pia mechi nyingine zitawahusisha JKT Tanzania dhidi ya Mtibwa Sugar
uwanja wa Isahmuhyo, Ndanda dhidi ya Singida United, Mbeya City dhidi ya Ruvu
Shooting na Mbao itamenyana na Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment