UONGOZI wa
Ruvu Shooting umesema kuwa msimu huu wa mwaka 2019/20 wamejipanga kuushangaza
ulimwengu wa mpira kwa kutwaa kombe la ligi lililo mkononi mwa Simba.
Ruvu
Shoting ilishinda mchezo wake wa kwanza mbele ya Yanga ikiwa ugenini kwa
ushindi wa bao 1-0 na kuvunja rekodi iliyodumu kwa muda wa misimu 9 ambapo Ruvu
Shooting ilikutana na Yanga mara 18 na ilipoteza jumla ya mechi 15 na sare
tatu.
Bao pekee lililoipa ushindi Ruvu Shooting lilipachikwa kimiani na Sadat Mohamed akimalizia pasi ya Hassan Dilunga, uwanja wa Uhuru.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa
wamejipanga kufanya maajabu ambayo yatashangaza ulimwengu kwa kutwaa kombe la
ligi.
“Hapa hakuna
cha Simba wala Yanga, kazi ndo imeanza kwa sasa hawa Yanga tuliwaambia
wameponzwa na ubishi wao ni salamu kwa walioshikilia ubingwa kwamba mwendo wetu
mpaka tunautwaa ubingwa msimu huu,” amesema Bwire.
Lugha kama hiyo waliitumia Yanga dhidi yenu na leo unaitumia Kwa wengineo. Ni mspema Sana kutamba usubiri kidogo kwasababu Kiki ndio inaanza. Mwaka Jana Mbao, Mtibwa na Azam waliongoza vizuri mwanzoni
ReplyDelete