September 3, 2019



MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mchezaji wake David Molinga ‘Mwili Jumba’ sio wa kawaida ana vitu vya kipekee ambavyo ataonyesha mbele ya ligi.

 Molinga ni mshambuliaji mpya wa Yanga amejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea timu ya AC Lega ya Congo amechukua nafasi ya Heritier Makambo aliyetimkia AC Horoya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa,kushindwa kufunga kwa mchezaji haina maana hajui bali ni mazingira kumkataa na kukosa utulivu kwakwe kunamponza.

“Nina amini Molinga atafanya mambo makubwa ndani ya timu hasa ukizingatia tayari ameshaanza kuzoeana na wachezaji wenzake kilichobaki ni kuona matokeo kwake.

“Ligi ina michezo mingi hauwezi kutoa hukumu kwa kutumia mchezo mmoja hiyo sio sawa bado ana nafasi ya kufanya vizuri na uwezo wake utakuwa wazi kama ilivyo mchezo wa mpira akipata utulivu na mazoezi atakuwa vizuri kama ilivyokuwa kwa Makambo” amesema.


1 COMMENTS:

  1. Ningependa kutoa ushauri ufuatao:
    1. Kufanya UHARAKA katika utekelezaji wa mambo mengi mfano UKARABATI NA UJENZI WA JENGO LA KLABU NA UWANJA WA MAZOEZI....KUMEKUWA NA AHADI NA UZITO WA KUFANYA UJENZI....
    2. KUFANYA HARAKA UJENZI WA MRADI WA KIGAMBONI YANGA COMPLEX....KUMEKUWA NA UZITO NA KUSUASUA
    3. Uhamasishaji kuelekea mechi ya tarehe 14 uanze sasa hivi...kumekuwa na siasa na ahadi bila ya vitendo
    4. Uingizaji ama uandikishaji wa wanachama na wapenzi wapya wa Yanga nchi nzima umebaki kuwa mipango tu hakuna utekelezaji
    5. Kubadilishwa kwa mfumo wa uendeshaji kutoka umiliki wa 100% kwa wanachama na kuingia soko la hisa (51% wanachama , 49% wawekezaji wasiopungua 3)...utekelezaji umekuwa mdogo ama unasuasua au hautangazwi kuujulisha umma ulipofikia na kwanini auendelei?

    Ahsante

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic