KUTOKANA na kazi aliyofanya jana uwanja wa Taifa kwa kuokoa penalti moja na kuwapotezea uwezo wa kujiamini na akukosa penalti mbili sasa Juma Kaseja anaongelea minoti ya kutosha.
Stars jana iliibuka kidedea mbele ya Burundi kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia kwa ushindi wa penalti 3-0 baada ya dakika 90 120 kukamilika kwa kufungana bao 1-1.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameandika namna hii kwenye ukurasa wake wa Instagram:"Kwa kweli Mungu anazidi kutuonyesha upendo wake Hongera watanzania hongera Taifa.
" Kama tulivyoongea usiku pale Hyatt hotel wachezaji wote mmetimiza kiapo chenu nami nawaomba kwa muda wenu nitimize kiapo changu kwenu.
" Mwisho kila mchezo una nyota naomba nimpatie Milioni 10 ndugu yetu Juma Kaseja kama nyota wangu,".
Hongera Taifa stars ila twendako ni kuzito zaidi hivyo kunahaja kwa wahusika kukitathmini kikosi kwa undani zaidi ili kuwa na timu ya ushindani na sio ya ushiriki tu. Vile vile wahusika wa Taifa wasichoke kufanya usahili wa wachezaji kila pale wanapoona mapungufu au kumuongeza mchezaji atakaeleta ushindani zaidi ndani ya Taifa stars. Binafsi nashngaa kwanini Muzamiru Yasini bado hajajumuishwa na kikosi cha Taifa stars ni mchezaji mwenye kujituma mwanzo mwisho.
ReplyDeletemtazamo mzur
Delete