YANGA HII LAZIMA UKAE, YAIONESHA JEURI SIMBA, MABILIONI HAYA YAINGIZWA
Uongozi mpya wa Klabu ya Yanga ulioingia madarakani chini ya mwenyekiti wake, Mshindo Msolla na makamu wake, Frederick Mwakaleba umefanikiwa kukusanya shilingi 3,935,000,000 ndani ya miezi minne tangu walipoingia madarakani.
Viongozi hao waliingia madarakani Mei 5, mwaka huu baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
Msolla na Mwakalebela kabla ya kuingia madarakani katika kampeni zao waliahidi kuipambania klabu hiyo kwa kuhakikisha wanaongeza vyanzo vya mapato kupitia udhamini mbalimbali wa makampuni.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Championi Ijumaa, Yanga hadi hivi sasa ina udhamini wa makampuni saba ambayo yote yamemwaga mamilioni na mabilioni ya fedha.
Makampuni na viwango vya fedha walizomwaga ni Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa iliyoweka udhamini wa Sh bilioni 1.94 ambao umeboreshwa hivi karibuni baada ya viongozi hao kuingia madarakani wakati awali walikuwa na mkataba wa Sh Mil 970.
Kampuni nyingine ni GSM walioshinda tenda ya uuzaji wa jezi za Yanga iliyotoa Sh bilioni 1.3, pia kampuni hiyo imeongeza fedha kwa kutoa Sh milioni 150 ya udhamini kupitia magodoro yao ya GSM.
Wadhamini wengine ni Taifa Gas chini ya mfanyabiashara, Rostam Aziz ambapo wamekubali kutoa Sh 300m kwa ajili ya udhamini, ambapo tayari Yanga wameshaanza kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini huyo begani.
Dili lingine ni kuwa Azam TV wanaonyesha kipindi cha Yanga TV ambapo kupitia kipindi hicho Yanga wananufaika kwa kupata Sh milioni 100, udhamini mwingine ni Afya Maji wenye thamani ya Sh milioni 100 huku Vodacom wanaodhamini Ligi Kuu Bara wakiinufaisha klabu hiyo kwa Sh milioni 45.
Jumla ya udhamini wote ni Sh bilioni 3.93 ambazo viongozi hao wapya wamezipata ndani ya kipindi kifupi cha miezi minne.
Akizungumzia hilo juzi kwenye kikao cha viongozi wa matawi wa Yanga kilichofanyika kwenye Makao Mkuu ya Klabu ya Yanga, Msolla alisema: “Mpaka hivi sasa Yanga ina mkataba na Sportpesa ambao mwaka huu watatoa Sh bilioni 1.94.
“Uongozi umefanikiwa kupata mikataba na Taifa Gas kutoka kwa Rostam ambao watatoa milioni 300, lakini pia ushirikiano na mheshimiwa Rostam bado upo, ndiye aliyetoa Sh milioni 60 kuvunja mkataba wa Kindoki na fedha za kumleta Molinga Yanga.
“Mkataba wa kwanza na GSM ni ule wa jezi ambao klabu itapata shilingi 1,300 kwa kila jezi itakayouzwa na lengo ni kuhakikisha jezi milioni moja zinauzwa ili klabu ipate Sh bilioni 1.3, pia mkataba unahusisha ukarabati wa Jengo la Yanga.
“Mkataba wa pili na GSM unahusisha magodoro ya GSM mkataba huu una thamani ya milioni 150, pia klabu ipo mbioni kuongeza mdhamini mwingine kutoka kampuni ya vinywaji atakayetoa fedha kama ilivyofanya SportPesa na kukarabati ‘pitch’ ya Uwanja wa Kaunda uwe wa kisasa kutumika katika mazoezi, ndiyo maana zoezi la kuweka kifusi linaendelea kwa kasi,” alisema Msolla.








Tumeona Jana jinsi mabilioni yalivofanya kazi Kwa kuilaza timu ngumu ya Pamba Kwa droo
ReplyDeletemojamoja na Kwa ujasiri uleule muilaze Zesco ya Luandamila bila ya huruma na mupafike waliposhindwa Simba kupafikia
loloto laweza tokea nawashaur wajipange
ReplyDeleteMsiwapoze mashabiki Kwa mabilioni wapozeni Kwa viwango bora mashabiki wataka ushindi sio majisivu ya mabilioni kila kukicha. Timu haina kiwango tunashindania kutaka ubingwa sio mabilioni feki
ReplyDeleteUSHAURI NI KWA NAMNA IPI FURAHA IPATIKANE NA USHINDI URUDI YANGA
ReplyDelete1. TIMU KUIMPROVE UWEZO, MBINU NA KUSHINDA MECHI......JUKUMU BENCHI LA UFUNDI
Nilisema hapo mwanzoni na narudia kusema kwa nia ya kujenga....hili mashabiki wahudhurie viwanjani bila kuwashurutisha ama kuwajengea hamasa ni lazima timu iweze kucheza soka la kuvutia na kuwa na mbinu za uwanjani kuweza kupata matokeo mazuri kila mechi....kuna mapungufu kwenye benchi la ufundi, wachezaji na mipango ya mazoezi na mbinu kwa ujumla....inawezekana uwezo wa ufundishaji ukawa umefikia ukomo....hili linahitaji mjadala na utatuzi haraka sana kabla ya mambo hayajaenda kombo.
2. Mwalimu apunguze exposure (kujianika anika) kwenye vyombo vya habari na matukio mengi (harambee, mialiko ya kuonekana katika umati wa mashabiki, sikukuu za ufunguzi wa matawi, vipindi cha mahojiano na vyombo vya habari nk..) Ajikite zaidi kwenye fani yake ya kufundisha mpira....kifupi aishi ki-professional
3. Hii dhana ya kwamba timu ya wananchi...isipoangaliwa inaweza ikaleta dosari na kuruhusu maadui kuingilia misafara ya timu na kudhuru timu kwa njia mbalimbali.....lazima kuwepo na udhibiti kwenye kambi na mazoezini na hata kwenye mechi....msiruhusuruhusu hata wanaokuja kwa lengo la mahojiano na vyombo vya habari hili suala libaki kuwa jukumu la uongozi (Mratibu wa Timu au Meneja)
4. Wachezaji wawe na umoja na upendo
wenyewe kwa wenyewe na kuhimizana kucheza kwa ari na ushirikiano kwa manufaa ya timu...kushambulia kwa akili, mbinu na malengo sio kubutuabutua bora liende mbele.....viungo na mabeki kukaba bila kujisahau na kupunguza makosa makosa kwenye mechi....wachezaji kushirikiana kupunguza mianya ya makosa
5. Suala la Mwalimu Msaidizi ili kulipa nguvu benchi la ufundi na kuimprove performance ya timu (kwani ni dhahiri uwezo wa timu na mchezaji mmojammoja unashuka kwa kasi mno).....Hata kama 2/3 ya timu ni wapya....lakini haionekani improvement ya kucheza kitimu...
Ahsante
Al nakuunga mkono. Timu bado haionekani kucheza kwa mtiririko wenye kuleta picha kuwa kuna magoli yanaweza kupatikana. Mashambulizi yako too predictable hata Pamba fc yenye watu pungufu iliweza kuyazuia. Zesco wanatumia vema mipira ya krosi na mashuti ya mbali!natumai mwinyi zahera ana mpango madhubuti wa kutumia krosi za chini zaidi(sqr balls) badala ya juu kupata magoli! Na mabeki wake kuzuia hiyo mipira.
Delete