October 29, 2019


Achana na kufungwa kwa Yanga dhidi ya Pyramids FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho juzi, timu hiyo itamkosa beki wake Kelvin Yondani katika mechi ya marudiano.

Yondani alipewa kadi ya pili ya njano na nyekundu kutokana na kucheza madhambi, kitendo ambacho hakitamruhusu kuwa sehemu kutokana na kanuni za CAF.

Kukosekana kwa beki huyo mkongwe ambaye ana uzoefu katika mashindano ya kimataifa inaweza ikawa pigo kwa Yanga sababu ameshiriki mashindano mengi ya kimataifa.

Mtihani sasa unabaki kwa Kocha, Mwinyi Zahera namna ya kumtumia mbadala wake katika mechi hiyo itakayokuwa ya aina yake na ngumu kwa Yanga.

Inaelezwa Yanga wataondoka Alhamisi ya wiki hii kuelekea Misri kwa ajili ya mechi hiyo ya marudiano. 

3 COMMENTS:

  1. Kila la heri mtani kwa kipigo cha ugenini mana hakikwepeki, nendeni pia kwa ajili ya kufuata sheria za soka maana hapo ni kukamilisha ratiba tu. Hivi pale msimbazi kwenye msimamo wa VPL wako namba ngapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnanunua mechi nyie! Ni aibu kwa timu kubwa kama Simba kujikita kwenye kununua mechi badala ya kujenga timu. Kwa matokeo mnayoyapata haielezeki mtolewe na UD Songo- Wamachinga wamakonde wa mchumbiji.

      Delete
  2. CAF imetoa viwango vya soka barani Africa kwa club simba ikiwa ni ya 16. Hembu tuambieni nyie wa matopeni ni wa ngapi..kutaka kumlinganisha na simba wakati we ni mbweha.. ��

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic