October 4, 2019


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kuona kuwa kesho wanabeba pointi tatu muhimu mbele ya Namungo Fc kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa uwanja wa Azam Complex.

Azam FC imeshinda michezo yake yote miwili iliyocheza msimu huu, ilianza mbele ya KMC kwa kushinda bao 1-0 uwanja wa Uhuru na kumaliza na Ndanda FC kwa kuifunga mabao 2-0.

Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kikosi kipo tayari na hesabu ni kupata matokeo chanya.

"Kwa sasa timu zote ambazo tunacheza nazo zinajipanga na zinafanya vizuri kutafuta matokeo, tunatambua umuhimu wa kila mechi nasi tutapambana ili kupata matokeo chanya mashabiki watupe sapoti," amesema.

Mchezo huo wa Azam na Namungo utachezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1.00 usiku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic