Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche, amesema kuwa leo wanataka kuweka heshima mbele ya Simba kwa kuchukua pointi tatu muhimu.
Azam FC itamenyana na Simba uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wao wa kwanza msimu huu kwenye ligi.
Cheche amesema:-"Tunataka kurejesha heshima na kuhakikisha tunakusanya pointi kuelekea mbio zetu za kuchukua ubingwa (VPL) na kupata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.
"Kila kitu kipo sawa na morali ya wachezaji ni kubwa ni suala la kusubiri wakati, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Msimu uliopita Azam FC ilikusanya pointi moja mbele ya Simba kwani mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 na mchezo wa pili ililazimisha sare ya bila kufungana uwanja wa Uhuru.
Kagere na miraji athuman hawatacheza na bado ushindi upo.
ReplyDeleteMnajiboost ili kutengeneza mazingira ya kujitia moyo,ha ha ha ha kipigo hakiwezi kukuponya hatamfanye nin lazima mpigwe,this is simba brother.
ReplyDelete