October 12, 2019


Huku timu yake ya zamani ya Yanga ikipewa Waarabu kutoka Misri timu ya Pyramids FC, Heriter Makambo na timu yake ya Horoya AC wamepangiwa kucheza dhidi ya timu ya Bandari kutoka Kenya.

Makambo anayeitumikia Horoya AC ya Guinea, walitolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kutupwa katika mechi za mtoano za Kombe la Shirikisho Afrika sawa na Yanga.

Horoya AC waliondolewa na JS Kabylie ya Algeria huku Yanga ikitolewa na Zesco United kutoka Zambia.

Wakati Makambo akielekea Kenya, timu yake ya zamani Yanga itaanza kibarua cha raundi ya kwanza dhidi ya Pyramids FC kutoka Misri jijini Mwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic