DICKSON Daud, nahodha wa Mtibwa Sugar ameliondoa gundu la timu yake kushindwa kupata pointi tatu lililodumu kwa dakika 450 sawa na mechi tano ambazo Mtibwa Sugar walicheza bila kuambulia pointi tatu.
Mtibwa walifungua pazia kwa kichapo cha mabao 3-1 na Lipuli uwanja wa Samora, ikapoteza kwa Simba, uwanja wa Uhuru 2-1 ikalazimisha sare ya bila kufungana na JKT Tanzania uwanja wa Isahmuyo ikakubali kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Tanzania Prisons na ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City zote uwanja wa Jamhuri.
Dakika ya 15 Daud alivunja mwiko huo kwa kuifungia bao timu yake ilipokuwa ikicheza mchezo wake wa sita mbele ya Ndanda FC uwanja wa Nangwanda Sijaona na kufuta lile gundu la kukosa ushindi ndani ya dakika 450.
Zubeir Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa tatizo kubwa lilikuwa kwenye upande wa umaliziaji jambo ambalo linaanza kupata dawa taratibu.
Ndanda iliyo chini ya Kocha Mkuu Malale Hamsini inafikisha mechi yake ya tano sawa na dakika 450 bila kuonja ladha ya pointi tatu kwani imeambulia sare tatu na imepoteza mechi mbili.







0 COMMENTS:
Post a Comment