October 21, 2019


NAMUNGO FC inayotumia uwanja wa Kassim Majaliwa imeendeleza rekodi yake ya kucheza kwenye uwanja huo bila kupoteza huku wakiitibua rekodi ya Lipuli iliyocheza mechi nne sawa na dakika 360 bila kupoteza kwa kuifunga bao 1-0.
Namungo iliyopanda daraja msimu huu ilicheza mchezo wake wa nne bila kupoteza kwenye uwanja wake wa nyumbani ilianza kubeba pointi tatu mbele ya Ndanda kwa mabao 2-1, ikaichapa Singida United mabao 2-0 ililazimisha sare ya bila kufungana na Mwadui na kutibua rekodi ya Lipuli kwa kuifunga bao 1-0.
Lipuli iliyo chini ya Kocha Mkuu Herman Harman ilianza ligi kwa kasi baada ya kushinda mechi mbili mbele ya Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1 na ikishinda mbele JKT Tanzania kwa bao 1-0 iliambulia  sare mbili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons zote ilikuwa ni sare ya kufungana mabao 2-2.
Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amesema kuwa wachezaji wake wanatambua umuhimu wa kutumia uwanja wa nyumbani hasa wanapokuwa na mashabiki wao wanaowapa sapoti nao wanafanya kweli kutowaangusha.
“Hamna namna nyingine kwa wachezaji wakiwa nyumbani wanatambua umuhimu wa mashabiki, ugeni wetu kwenye ligi unatufanya tutumie nguvu nyumbani jambo litakalotujengea kujiamini zaidi tukitoka,”amesema Thiery.   
Bao la ushindi lilifungwa na Hashim Maanja linaifanya Namungo kuwa na pointi 10 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic