Imeelezwa kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewaarifu Yanga kuwa wanaweza kuwatumia wachezaji wake wawili ambao ni David Molinga 'Falcao' na Mustafa Seleman.
Taarifa imeeleza kuwa Yanga inaweza kuwatumia wawili hao katika mchezo wa Play Off dhidi ya Pyramids FC ya Misri Oktoba 27 mwaka huu.
Yanga itakuwa na kibarua cha raundi ya kwanza ya mashindano hayo na waarabu hao ambapo mechi ya kwanza itafanyika Tanzania.
Kwa taarifa za ndani, inaelezwa tayari CAF wapo katika mchakato wa kukamilisha suala la leseni za wachezaji hao ambao hawajacheza mechi yoyote ya kimataifa tangu wasajiliwe.
0 COMMENTS:
Post a Comment