MABONDIA wa
ngumi za kulipwa nchini, Issa Nampepeche na Ally Hamisi jana walipima uzito tayari kwa pambano la usiku wa mabingwa litakalofanyika leo kwenye Ukumbi wa Club 361 uliopo Mwenge, Dar.
Mbali
ya mabondia hao wengine watakaopima uzito kwa ajili ya pambano hilo ni Said Sudi atakayezichapa na Maganga Kulwa,
Ibrahim Makubi dhidi ya Abdallah Kingolwira, Hashimu Msungo vs Epson
Lewis wakati Salumu Omari atamalizana na Ramadhani Chicho huku
yakiwa chini ya udhamini wa Gazeti la Championi, +255 Global radio,
Smart Gin, Glady Matata na Kiwango Security.
Mratibu wa pambano hilo, Seleman Semunyu amesema kuwa
maandalizi ya pambano hilo yamekamilika ambapo na mabondia walipima uzito kwenye Ukumbi wa Club 361.
“Maandalizi yanakwenda vizuri kwa mabondioa
wote ambao watapanda ulingoni siku hiyo ambayo itakuwa ni kazi moja tu ya
kuwapongeza mabondia wetu ambao wamechukua mikanda ya ubingwa nje ya mipaka ya
Tanzania.
" Ijumaa mabondia wenyewe ndiyo watapanda ulingoni, kikubwa mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wajitokeze kwa wingi kushuhudia ngumi zikifanyika katika ustarabu wa hali ya juu kwa kiingilio kidogo,” amesema Semunyu.
0 COMMENTS:
Post a Comment