October 4, 2019


Jose Mourinho ametajwa kuwa ni mmoja wa wanaopewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Mauricio Pochettino katika kuinoa Tottenham.

Pochettino yupo katika presha kubwa baada ya timu yake kuchapwa ikiwa nyumbani mabao 7-2 na Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mbali na hapo Pochettino alishuhudia timu yake pia ikifungwa na timu ya Ligi Daraja la Pili ya Colchester United na kutolewa katika michuano ya Carabao Cup, wiki jana huku kwenye Premier League nako wakiwa wanayumbayumba.

Mourinho, 56, ambaye hana kazi tangu alipofukuzwa Man United, Desemba, mwaka jana anatajwa kuwa ndiye mtu sahihi kutokana na uzoefu wake kwenye timu kubwa.

Wengine ambao wanapewa nafasi ya kupewa mikoba ni kocha wa zamani wa Juventus, Massimiliano Allegri na kocha wa sasa wa Bournemouth, Eddie Howe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic