October 4, 2019


Kocha wa Simba, Patrick Aussems amechukua tuzo ya Ligi Kuu Bara kwa mwezi Septamba kwa kuwashinda Mohammed Rishard wa Prisons na Abdallah Mohammed Baresi wa JKT Tanzania, ambapo Aussems aliongoza timu yake kupata ushindi katika michezo mitatu.

Kati ya hiyo mmoja nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar na miwili ugenini mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar na mabao 2-0 dhidi ya Biashara United. Simba imemaliza mwezi ikiwa nafasi ya kwanza. 

Rishard aliingia hatua ya fainali baada ya kuiongoza Prisons kushinda michezo miwili na kutoa sare mmoja, ambapo ilishinda nyumbani mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, kisha ikashinda ugenini mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa na ikatoka sare ugenini na Lipuli ya mabao 2-2, wakati Baresi aliingoza JKT Tanzania kushinda michezo miwili, sare moja na kupoteza mmoja.

JKT Tanzania ilifungwa ugenini bao 1-0 na Lipuli,  ikatoka 0-0 nyumbani na Mtibwa Sugar,  ikashinda bao 1-0 ugenini dhidi ya Biashara United na pia ikapata ushindi ugenini kama huo dhidi ya Kagera Sugar.

1 COMMENTS:

  1. Welldone coach keep it up.Ushauri wa bure jaribu kuwarotate young players

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic