October 19, 2019


Ni kama hofu tena imeingia kwa baadhi ya mashabiki na wadau wa Yanga kutokana na wachezaji David Molinga 'Falcao' pamoja na Mustafa Suleiman kutokuwa sehemu ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC.

Yanga itakutana na timu hiyo ya Misri katika mechi ya raundi ya kwanza Oktoba 27 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, kabla ya kurejeana Novemba 03 mwaka huu.

Kufuatia kauli ya kaimu Mwenyekiti wa klabu, Fredrick Mwakalebela jana kuwa rasmi Yanga itawakosa wachezaji hao, baadhi ya mashabiki na wadau wameshangazwa na alichokisema kiongozi huyo.

Ikumbukwe hivi karibuni ilielezwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lipo katika harakati za mwisho kutuma vibali vyao na jana taarifa nyingine tofauti imetoka.

Wengi wameeleza kuwa inaweza ikawa changamoto tena kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga, ambapo wengi wanaamini Falcao anaweza akawa na mchango mkubwa.

Licha ya hoja hizo kuwepo, Mwakalebela aliweka wazi kuwa suala hio bado lipo kwenye mchakato na endapo Yanga wakitinga hatua ya makundi wataweza kuanza kazi rasmi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic