October 19, 2019


Ni kama nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi cha Simba inaenda kuongezeka kufuatia kurejea kwa straika na nahodha John Bocco aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Jana Bocco ameanza mazoezi mepesi chini ya kocha wa viungo wa klabu hiyo kabla ya kujumuika na wenzake katika mazoezi ya jumla.

Bocco alianza mazoezi hayo kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi ambapo tangu msimu huu uanze wa Ligi Kuu Bara hajacheza mechi yoyote ya ligi.

Bocco atafanya mazoezi hayo maalum peke yake kwa takribani wiki moja na baada ya hapo atajumuika na wenzake kwa mazoezi ya ujumla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic