KISA WAARABU, YANGA YASHUSHA MTAALAMU MPYA
Ili kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kabla ya kuwavaa Waarabu, timu ya Pyramids kutoka nchini Misri, uongozi wa Yanga umeongeza nguvu katika benchi la ufundi kwa kumleta daktari mwingine.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa, wameongeza nguvu katika upande wa madaktari ili kupunguza majeruhi yasiyokuwa ya lazima.
“Tumeongeza nguvu upande wa madaktari ambapo kuna baadhi ya madaktari tumewaongeza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi dhidi ya Pyramids ili kupunguza majeruhi ambayo yatakuwa si ya lazima.
“Madaktari watakuwa karibu na kila mchezaji kwa kuwaangalia mmoja mmoja ili kuhakikisha wanajilinda tukiwa na lengo la kumsaidia kocha, Mwinyi Zahera aweze kuwa na kikosi kipana kitakachomsaidia.
“Wachezaji ambao walikuwa majeruhi wanaendelea kuimarika na wanapatiwa matibabu kwa ukaribu zaidi kuhakikisha wanakuwa fiti haraka,” alisema Mwakalebela ambaye amewahi kuwa kiongozi wa Mtibwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).








Kifo hakiepukiki hata kama una madaktari 100 . Rais Tito wa Yugoslavia alikuwa na daktari kwa kila kiungo cha mwili wake , lakini alipougua kifo hakikukwepeka. Yanga nawashauri muwekeze katika mazoezi ya kupambana na mbao na sio kuongeza madaktari kwa maandalizi ya kuwakabili Pyramids ambao sio size yenu
ReplyDeleteUmeongea ukweli kabisa kaka Selemani Sindano,saizi ya Yanga ni UD Songo na sio hao Pyramid!
Delete