KOCHA ARSENAL ATIA MGOMO JUU YA OZIL, HIZI NI TETESI ZA LEO IJUMAA
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Lukas Podolski ametoa kauli ya kebehi kwa wapinzani wake wa zamani Tottenham kwa kusema kuwa Serge Gnabry inabidi awe mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal. Gnabry ambaye amewahi kuichea Arsenal alifunga goli nne peke yake wakaqti Bayern ikiidondoshea Spurs goli 7-2 wiki hii.
Kocha wa zamani wa England Fabio Capello amefichua kuwa alijaribu kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi kwa mkopo kipindi akiinoa timu ya Juventus. (Sky Sports Italia via Mail)
Mchezaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33, na Callum Wilson, 27, wa Bournemouth wapo katika rada za usajili wa klabu yaManchester United ambao wanatafuta kwa nguvu zote mshambuliaji wa kusajili katika dirisha dogo la mwezi Januari. (Sky Sports)
Kiungo nyota wa Norway Martin Odegaard, 20, anapanga kurejea Real Madrid japo klabu za Manchester United na Liverpool. Kiungo huyo kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Real Sociedad. (Goal)
Kiungo nyota wa Tottenham Christian Eriksen bado anaamini mipango yake ya kuhamia Real Madrid inaweza kufanikiwa, na wakala wake mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kwenda Uhispania kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Madrid. (Star)
Real Madrid walifikiria kumteaua Antonio Conte kuwa kocha wao mwaka jana, kabla ya kocha huyo wa zamani wa Chelsea kurudi dimbani na klabu ya Inter Milan. (Fichajes.net, via Calciomercato)
Klabu ya soka ya LA Galaxy ya Marekani inaripotiwa kumnyemelea mshambuliaji wa klabu ya Rangers ya Uskochi na raia wa Colombia Alfredo Morelos, 23. (Star)
Kocha wa Arsenal Unai Emery amegoma kukanusha uwezekano wa kiungo Mesut Ozil kuihama klabu hiyo mwezi Januari. (Sun)
Kocha wa zamani wa Brighton Chris Hughton amekataa ofa ya kuinoa klabu inayosuasua ya daraja la kwanza, Stoke City. (Mirror)
0 COMMENTS:
Post a Comment