KOCHA SIMBA AIONDOA YANGA CAF
Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa hana imani kabisa na Yanga kama itashinda mbele ya Pyramids FC kwa kuwa hawako kwenye kiwango kizuri tangu msimu umeanza.
Yanga imepangwa kucheza na Pyramids FC ya Misri ambapo mchezo wa kwanza itacheza Oktoba 27 kisha marudiano Novemba 3, mwaka huu.
Hii ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuchezesha droo ambapo michezo ya mtoano imepangwa kuwania kufuzu Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Ukweli sina imani na Yanga, sababu kiwango chao kwa sasa siyo bora wanashindwa tu kutamba mbele ya Ruvu sijui Coastal ndiyo wakapambane na hao Pyramids, sidhani kama watafanikiwa kwa hilo.
“Yanga kwa sasa ina wachezaji lakini hawana muunganiko, timu haijawa sawa kabisa kusema inaenda kushindani na Mwarabu ambao kwa fitina ndiyo sehemu yao, siyo rahisi kwa wao kusonga mbele, niwe muwazi tu.
“Pia wanatakiwa kuweka mambo yao sawa hasa yale ya ndani, kuvurugana waache, zaidi wapambane kujenga timu ambayo itakuwa inaeleweka wakisema hii ni Yanga hujiulizi mara mbili,” amesema Julio.
Yanga ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika Raundi ya Kwanza dhidi ya Zesco United kwa jumla ya mabao 3-2.
Julio umesema maneno ya maana sana wanatakiwa kujithamini kabla ya kuanza kupiga kelele
ReplyDeleteYanga hata akipeleka mechi uwanja wa Manungu ataoigwa tu.Yanga inacheza mpira wa magezetini
ReplyDeleteMbona mnaocheza mpira uwanjani mbona hatuwoni mchezea wapi ? Acheni unafiki hata hiyo timu yenu nimbovu ndio maana Leo hii na cheza na bandari
ReplyDeletehao ndo mbumbumbu fc' bado wanaweweseka na ud songo
DeleteWell said Julio,nakubaliana na maoni ya Jamhuri japokuwa hatupendi kuambiwa ukweli lakini ni jambo lililo dhahiri machoni mwa wapenzi wa Yanga
ReplyDeleteWapuuzi FC nawaonea huruma. Kipigo kama kawaida. Mpira unachezwa ndio maana tuna pointi 12 na nyie man 4 tena za kubebwa. Safari hii zinashuka timu 6 endelezeni ngebe na visingizio mtajikuta mnacheza daraja la kwanza mwakani.Hivi sasa mko wa ngapi 16 au?
ReplyDeleteHivi kwa akili zako hizo unaiwazia Yanga kushuka daraja
Delete