October 12, 2019


Na George Mganga

Aliyewahi kuwa mchezaji na Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amemshangaa beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' kugoma kuitumikia timu hiyo sababu ya kudai fedha zake zake.

Dante ameingia katika mgomo wa muda mrefu kuichezea Yanga mpaka ikafikia hatua ya kujiondoa kwenye program za timu hiyo, kutokana na kutolipwa fedha zake ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 40.

Julio amesema kitendo cha Dante kudai fedha huku akiwa hachezi mpira anakuwa anajiharibia mwenyewe na kinaweza kumletea matatizo siku za usoni.

Ameeleza kuwa wachezaji wengi wa kitanzania wamekuwa na changamoto kama za Dante lakini si sababu ya yeye kuacha kucheza mpira kwani atapotea katika ramani ya soka.

"Unajua wachezaji wengi wa kitanzania wana changamoto kama hizo, kuacha kucheza sababu ya kudai ni kujiharibia mwenyewe.

"Ukiangalia wachezaji wengine kama Mbwana Samatta, alicheza Simba na baadhi ya ahadi alizoahidiwa hazikutimizwa lakini alipambana kwa kuvumilia na sasa amefika mbali.

"Namshauri Dante arudi akazungumze na mabosi wake wayamalize, aanza kazi na watamlipa kidogokidogo kama ambavyo wamekuwa wakisema.

"Asikae tu nyumbani kisa anadai, si yeye peke yake, kucheza ndiyo itamfanya yeye alipwe na itamsaidia kulinda kiwango chake."

Takribani siku nne zilizopita uongozi wa Yanga ulisema upo tayari kumlipa Dante fedha zake kwa mafungu, ingawa mchezaji mwenyewe alikataa na kutaka alipwe zote kwa ujumla.

6 COMMENTS:

  1. Acha uongo Julio nakumbuka Samatta aligoma kucheza karibu nusu msimu kwa sababu wakati anasainishwa mkataba kutoka African Lyon kuja simba aliahidiwa gari na hakupewa. Baada ya kukabidhiwa ndyo akajiunga na timu. Hivi mbona sijawasikia mkiwalaumu viongozi? Yaan kwa kuwa mpira ni kazi yake ndyo mnamdharau? Wakati mnakubaliana bei mlimjulisha kuwa hali ni ngumu tutakulipa kwa mafungu? Yaani watu wamepiga kazi enzi za njaa kali mpaka Lwandamina alikimbia leo kuna neema mnawarundikia mamilion akina sibomana, balinya, molinga nk bado mnamwona Dante msaliti. HII NI DHARAU

    ReplyDelete
  2. Umeandika cha maan bro wazawa hawapew priority sana halaf kutumia heading ya kusema kocha wa simba ilimrad muuze gazet sio saf sema aliekuwa hapo utaeleweka

    ReplyDelete
  3. hivi kumbe George ni wewe ndiye unaandika upuuzi huu ndani ya hii blog.Mara nyingi topiki zilizoandikwa hovyo na kiholela hazina jina....Sio sawa na Bin Zuberi kule tunajua mwandishi ni nani.
    Cha kwanza Julio sio kocha Simba ...si sawa kuandika kocha simba kwani kabla ya kusoma habari ndani watadhani unaongelea Aussens...Pia humtendei haki kwani Julio hajawa kocha Simba tu...na labda kuna timu zingine alichezea mbali na simba.
    Yaani ulivyoandika hili ni kama vile Yanga hawana makosa...unawafagilia vizuri katika habari hii..
    Pili ni vigumu kuamini kuwa Julio atatoa ushauri kama huo "eti wewe kutocheza unajiharibia na anakuwa hana kipato kwani halipwi"
    Hii pia inawaharibia Yanga, Sababu za Lwandamila na Kamusoko kuondoka Yanga zinajulikana...ni madai madai kama haya...
    Kakolanya alidai hivi hivi kwa hiyo na yeye ameharibu...Sasa huu upuuzi anaofanyiwa Dante mbona Yondani hafanyiwi!.Ni aibu kushindwa kulipa mil 45 wakati michango na tileti za uwanjani zinaingiza mamia ya milioni.Jifunze kuandika George...kumbe ni wewe unaandika upuuzi

    Baadae kaandike kuhusu rekodi andika hata

    Simba imeizidi Yanga rekodi kwa kona iliyopigwa ikaingia moja kwa moja golini

    ReplyDelete
  4. Samatta aligoma ndipo akapewa gari.Wacheni uzushi wa kutosema kweli.Huyu kocha msema hovyo alikuambia nini Dodoma FC kama yeye uvumilivu?Wacheni kunywa pombe huku mnahubiri watu wanywe maji. Semeni ukweli .Andikeni ukweli.Mganga mapenzi kwa kandambili yamekufanya uwe mjinga. Unaandika upuuzi.

    ReplyDelete
  5. ulichaandika ni upuuzi...yaani haiingii akilini na ni wanafunzi wa shule ya msingii kuanzia la nne kurudi chini wanaweza amini ulichoandika...

    nikushauri Mganga rudi kwenye staili yako ya kuandika bila kuweka jina.leo umeumbuka..Tuandikie chochote basi kuhusu rekodi ya timu fulani kuzidi nyingine...
    HATA REKODI YA TIMU FULANI KUONGOZA KWA KUCHEZA SHAMBA LA BIBI...
    Hivi unajua unapotuandikia maandishi yeyote ni sawa unatufungulia njia tujue kiwanga cha akili yako..Ni sawa na shule unaandika mwalimu anaona huyu ni smart anatoa A...Ulichoandika Mganga kinastahili F! Tunaomba usifute hii habari au kwa kuishusha chini ikarudi imabadili kichwa cha habari

    ReplyDelete
  6. Na pia si kila kitu cha kuandika ww kama mwanataaluma unatakiwa kuandika kitu kwa weledi ili kujiongezea credit! Tendea haki professional yako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic