NYOTA wa mpira wa Kikapu, Kevin Durant ambaye alisepa kutoka timu ya Golden State na kujiunga na Brooklyn Nets kwa kulipotezea dili la Knicks amedai kuwa ilitokana na timu hiyo kukosa mvuto.
Wachambuzi wengi waliamini nyota huyo angemwaga wino kwenye timu hiyo na badala yake ikawa tofauti licha ya kupewa dili mezani.
"Mashabiki wakongwe wanakumbuka Knicks ilivyokuwa na nguvu na mvuto kiasi cha kufika fainali 1999, lakini wachezaji wa sasa hawajaliona hilo.
"Vijana wamekuwa wakiiona Golden State na LA Lakers kuwa ndizo timu kubwa, huwezi kwenda kwenye timu yenye jina kubwa lakini haina vipaji vinavyoendana na hadhi ya timu, siyo kwamba nawavunjia heshima lakini huo ndio ukweli," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment